Kenya yatangaza idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa Corona Kwa Kipindi Cha Masaa 24

Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe leo Jumatano Mei 27 ametangaza watu 123 zaidi kuambukizwa virusi vya corona.

Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya corona kuwahi kutangazwa kwa siku moja nchini humo tangu ugonjwa huo uingie Kenya mwezi Machi.

Mpaka kufikia sasa Kenya imethibitisha watu 1,471 kuambukizwa virusi hivyo.

Waziri Kagwe pia ametangaza watu watatu zaidi wamefariki kutokana na corona katika saa 24 zilizopita na kufanya watu waliopoteza Maisha kutokana na virusi hivyo nchini Kenya kufikia 55.


from MPEKUZI

Comments