Vifo vya Corona Duniani Vyapindukia Laki 2 Huku Marekani Ikiendelea Kuongoza

Marekani imeendelea kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ambapo hadi sasa watu 987,322 wameambukizwa virusi vya Corona nchini humo na 55,415 wamefariki dunia huku waliopona wakiwa 118,781

Nchi ya Italia inashika nafasi ya pili kwa idadi ya vifo vya Corona ingawa kwa upande wa maambukizo Uhispania imeipiku. 

Nchi za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinafuata kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ya virusi vya Corona, na kulifanya bara la Ulaya kwa sasa kuwa kitovu cha virusi hivyo.

Kwa upande wa Afrika nchi ya Afrika Kusini ni ya kwanza kwa idadi kubwa ya maambukizo ya virusi vya Corona ambapo hadi sasa kesi 4,546 za virusi vya Corona zimethibitishwa nchi humo huku watu 87 wakifariki dunia kwa ugonjwa  huo na waliopona ni 1,473

Takwimu za leo asubuhi  zinaonyesha kuwa, watu 2,996,562 wameambukizwa virusi vya Corona kote ulimwenguni na hadi sasa watu  207,023 wameshaaga dunia kwa ugonjwa huo huku 881,845  wakiwa wamepona


from MPEKUZI

Comments