Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba China inampango wa kutumia kila njia ili kumfanya asichaguliwe tena kwenye uchaguzi mkuu wa Urais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu
Katika mahojiano yaliofanyika katika Ikulu ya Whitehouse na chombo cha habari cha Reuters, amesema kwamba China inakabiliwa na athari chungu nzima kutoka kwa Marekani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Anasema China ilificha kuhusu ugonjwa wa Corona na hivyo kuufanya usambae dunia nzima na kuleta madhara makubwa.
Hata hivyo, Trump yeye mwenyewe amekuwa akikosolewa vikali kwa Jinsi anavyokabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo, Trump yeye mwenyewe amekuwa akikosolewa vikali kwa Jinsi anavyokabiliana na tatizo hilo.
Mlipuko wa virusi vya corona umeharibu uchumi wa Marekani ambao Trump alikuwa akitumia kama kinga kujipigia debe ili kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.
"China inafanya kila mbinu za kutaka nishindwe katika uchaguzi ujao. Wanataka mpinzani wangu mkuu kutoka chama cha Democrat Joe Biden ndo ashinde uchaguzi wa mwezi Novemba."-Trump
Aidha, Trump amepinga vikali utafiti uliofanyika nchini humo na kutoa maoni kwamba mpinzani wake Biden ana asilimia kubwa za kuibuka mshindi.
"Siamini kura hizo za maoni....Naamini raia wa taifa hili ni watu werevu. Na sidhani kama watamchagua mtu ambaye hawezi kuwasaidia kutatua changamoto zao''. -Trump
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment