Trump Aitishia China Kulipa FIDIA Kisa Corona

Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda nchi hiyo ikaitaka China kuilipa fidia kutokana na janga la maambukizi ya Corona kwa kile anachosema kuwa nchi hiyo ilishindwa kuzuia maambukizi ya Corona.

Trump amesema kwa sasa uchunguzi dhidi ya China unaendelea wakati huu nchi hiyo ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo vya watu zaidi ya elfu 56.

Hivi karibuni Rais Trump alililaumu shirika la Afya Duniani kwa kuegemea zaidi upande wa China.

Rais huyo wa Marekani alidai kwamba shirika hilo la kimataifa lilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais Trump alisema shirika hilo liliisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya Corona.

Tangu aingie madarakani Rais Trump amekuwa anayatilia mashaka mashirika ya kimataifa na mara kwa mara amekuwa analibeza shirika  hilo la afya. 

Katika bajeti ya mwezi Februari utawala wa Trump ulipendekeza kupunguza mchango wa fedha wa Marekani kwa shirika la WHO kutoka dola milioni 122.6 hadi dola milioni 59.9


from MPEKUZI

Comments