Baada ya Serikali kujenga Masoko ya Madini katika mkoa wa Madini Kahama ili kudhibiti biashara holela na utoroshwaji wa dhahabu imesaidia kuongeza Mapato ambapo kwa kipindi cha Julai 20 2019 hadi Aprili 2020 jumla ya shilingi bilioni 61.5 sawa na asilimia 77.62 zilikusanywa.
Hayo yalibainishwa Aprili 25 Mwaka huu na Afisa Madini wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu baada ya kuzungumza na Mwandishi wa habari kuhusiana na hali ya ukusanyaji wa Maduhuli ya serikali baada ya kuboreshwa kwa masoko ya Madini mkoni humo.
Alisema, fedha hizo zimetokana na Malipo ya Maduhuli ya mirahaba pamoja na ada za ukaguzi wa Makinikia katika migodi midogo na mikubwa ambazo zinakusanywa kwenye Masoko na miyalo ya Uchejuaji wa madini.
“Hapo awali wachimbaji na Wafanyabiashara ya Madini walikuwa wakiibia serikali kwa kuuza madini kwa njia za panya na kusababisha serikali kokosa mapato,lakini kwasasa baada ya kujenga masoko katika maeneo ya Kahama,Kakola Mwime,Mwazimba na Mwabomba yamesaidia kuongeza ,mapato kwa asilimia 77.62,” alisema Kumburu.
Kumburu alifafanua kuwa kwa sasa wafanyabiashara na wachimbaji wa Madini wameelewa faida za kuuza kwenye masoko kwani wanaweza kuuza kwa bei ya juu ikilinganishwa na hapo awali ambapo walikuwa wakitapeliwa na madalali kwa kuuza mali zao kwa bei ya chini.
“Sheria kali zinaendelea kuchukuliwa kwa wachimbaji ama wafanyabiashara wa madini ambao wanafanya biashara hii nje ya masoko,nitoe rai kwao kwani ukikamatwa madini yako yatataifishwa na wewe kuchukuliwa hatua kali za kisheria ni vyema mkauza ndani ya masoko yaliyotengwa na serikali,”alisema Kumburu.
Sambamba na hilo Mhandisi kumburu aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanaosha mawe yenye madini katika mialo ambayo inatambulika kisheria kwa kuwa na fomu za kujaza kiwango cha dhahabu ili kuepuka usumbufu pindi ukaguzi unapofanyika.
Mwandu Makoye ni mmoja wa Wafanyabiashara wa Madini mkoani humo ameipongeza serikali ya awamu ya Tano chini Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuanzisha masoko hayo na kusema kuwa kwa sasa wanapata faida kuwa ikilinganishwa na hapo awali ambapo biashara hiyo ilikuwa imeingiliwa na matapeli.
“Sisi kama wafanyabiashara Tunampongeza Rais wetu Magufuli kwa kutambua mchango wa sekta ya Madini,tunaahidi kufanyabiashar hii kwa uaminifu mkubwa na tupo tayari kuwafichua wenzetu ambao wamezoea Magendo katika sekta hii ya Madini.
Kabla ya kuanza kwa masoko hayo katika mkoa wa Kimadini Kahama Serikali ilikuwa inakusanya shilingi milioni 593,689,214.67 za mrahaba huku ada za ukaguzi wa Madini zikiwa ni shilingi milioni 8,481,274,495.27 kwa mwaka.
Mwisho.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment