Diamond atangaza kuzilipia kodi familia 500 zilizoathirika na Corona kwa miezi mitatu

Msanii wa mizki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametangaza kuwalipia kodi watu 500 walioathirika na Corona kwa miezi mitatu kila mmoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika ujumbe huu.

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara….nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba….🙏🏼
#HiliNaloLitapita#ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona
.
.
(I pretty much know that at these terrible times where we are all fighting global pandemic COVID-19,countless life circumstances have changed especially in businesses, many businesses are drowning hence rendering to financial difficulties and life becoming a little bit tough to many of us. Although I am amongst those affected by this pandemic on Economy, with the little that God has blessed me with, I have decided to atleast offer a helping hand by paying 3 Months house rent to 500 families as my kind gesture of helping one another during these terrible times of fighting COVID-19 for I believe i should share your troubles and your happiness too. On Monday i shall announce procedure on how these 500 families shall receive house rent. 🙏🏼)”


from MPEKUZI

Comments