Rais Magufuli amtumbua balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Rais ameyasema hayo leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma alipokuwa akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti za ukaguzi zilizoandaliwa na ofisi ya Madhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, pamoja na ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

“Mmetusaidia [TAKUKURU] kwa ripoti yenu kuhusu wizi wa mabilioni uliofanywa na ubalozi wetu wa Ethiopia, na balozi wa Ethiopia nimeshamrudisha, si balozi tena kule,” amesema Magufuli.

Amesema uamuzi huo uwe fundisho kwa watumishi wengine kwamba kiongozi akiharibu kwenye ofisi yake ajiandae kubeba msalaba.

Aidha, amewaomba viongozi wenzake kuitumia ripoti ya TAKUKURU ya mwaka unaoishia Juni 2019 kurekebisha yale yaliyotajwa, yakiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma na manunuzi bila kuwa na mkataba.


from MPEKUZI

Comments