Mbowe ajiweka Karantini baada ya mtoto wake kuthibitika kuwa na Corona

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amejiweka karantini siku chache baada ya kutangaza kuwa mwanaye Dudley amepata maambukizi ya Corona

Mbowe amesema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na hivi sasa yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama naye ana Virusi hivyo.

Akiongea na Clouds Media Mbowe amesema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na Corona ili aliokutana nao pia wawe salama.

Aidha, Mbowe ameeleza kuwa mkakati wa pamoja unahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona ambao amesema ni suala ya kitaifa.


from MPEKUZI

Comments