Wakazi wanne wa kitongoji cha Ngilimba ‘B’ kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wamefariki dunia baada ya kuvuta hewa yenye sumu iliyosababishwa na mkaa waliouwasha kwenye jiko na kisha kuliweka ndani ya nyumba yao ili kujikinga na baridi.
Akungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 28 mwaka huu ambapo wanafamilia hiyo waligundulika kupoteza Maisha ndani ya nyumba yao wakiwa wamelalala baada ya kuvuta hewa yenye sumu.
Kamanda Magiligimba aliwataja waliofariki dunia ni pamoja Masanja Emmanuel (35) ambaye ni baba wa familia hiyo, Mngole Masanja (25) mkewe, Holo Masanja,(05) na Matama Masanja (03) wote wakazi wa Ngilimba.
“Tukio hili limesababishwa na mvua iliyonyesha Machi 27 iliyoambatana na baridi kali ndipo marehemu hao waliamua kulala na jiko la mkaa ndani ya nyumba yao na kusababisha mgandamizo wa hewa kuwa mdogo uliosababisha wavute hewa yenye sumu ya carbon monoxide”,amesema Magiligimba.
Miili ya marehemu hao imekabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
Mwisho.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment