Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amefikishwa mahakamani mkoani Singida na kusomewa mashitaka 15.
Tarehe mbili mwezi huu, Lema alikamatwa na polisi mkoani Arusha na kusafirishwa hadi mkoani Singida ili ahojiwe, baada ya kutuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni kati ya mwaka 2019 na mwaka huu.

Kati ya mashtaka hayo moja ni la kusababisha taharuki kwa jamii na 14 ya kupotosha jamii.
Amesomewa mashtaka hayo leo Jumatano Machi 25, 2020 na mawakili wa Serikali, Monica Mbogo, Rose Cholongola, Michael Ng’hoboko na Caren Malando mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano.
Lema anadaiwa kutenda makosa hayo Februari 29, 2020 mjini Manyoni mkoani Singida katika mazishi ya kiongozi wa Chadema.
Anadaiwa siku hiyo na katika mitandao ya kijamii alisambaza taarifa za uongo kwa nia ya kupotosha jamii kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa mkoani Singida.
Lema alikana mashtaka yote yanayomkabili na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 huku mbunge huyo akiachiwa kwa dhamana.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment