Chad imetangaza siku tatu za mambolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya askari wake 98 waliouawa katika shambulio la Boko Haramu katika makabiliano ya Jumatatu Machi 23 katika Mkoa wa Lac.
Makabiliano hayo ni moja ya makabiliano mabaya kwa upande wa jeshi la Chad, kwa mujibu wa rais Idriss Déby.
Kikosi cha jeshi la Chad kilishambuliwa kwa kushtukizwa kwenye maeneo manne ya kivita. Wanamgambo wa Boko Haram ambao walikuwa na taarifa zote, hawakuwapa nafasi askari wa Chad kuweza kujibu. Na wakati kikosi cha askari wengine walikuja kutoa msaada walipofika katika kijiji cha Kaïga Kindjira, walijikuta wameshambuliwa bila hata hivyo kujibu, huku wapiganaji wa Boko Haram wakichukuwa silaha zote, na kuchoma moto magari kadhaa kabla ya kurudi nyuma.
Kwa mujibu wa rais wa Chad, kitengo cha askari walioshambuliwa walivamiwa kabla ya shambulio hilo. Hii inaelezea udhaifu wa jeshi la Chad dhidi ya kundi la Abu Musab al-Barnawi, kiongozi wa tawi la kundi la Boko Haram linalotambuliwa na kundi la Islamic State.
Kutokana na hali hiyo, msafara wa jeshi la Chad, waliokuwa njiani kuelekea Niger ili kuungana na wenzio katika eneo la mipaka mitatu kati ya Mali, Burkina Faso na Niger, walirejeshwa nyuma kwa kusubiri marekebisho kadhaa katika jeshi kama ilivyotangazwa Jumanne wiki hii na rais Idriss Déby.
Idriss Déby alitumia helikopta kwa kuzuru Bouma. Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Chad kukiri kupata hasara kubwa katika mkoa huo.
Wakati huo huo rais Idriss Déby amesema amechukuwa hatua kutoka na hali hiyo: "Nimeshuhudia operesheni nyingi, lakini kupoteza askari wengi mara moja ni mara ya kwanza katika historia yetu. Nimechukizwa kabisa na hali hiyo. Tutachunguza jeshi letu lote ili kuepukana na kile kilichotokea Bouma. "
Credit: RFI
Credit: RFI
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment