Zheng Rongman na mkewe, Ou Ya wote raia wa China wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Dola 5,000 za Kimarekani sawa na Sh11.5 milioni kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA), Dk Edwin Mhede.
Rongman ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co Ltd na mkewe wamekiri kutaka kutoa rushwa kwa bosi huyo wa TRA. Wanandoa hao ni wakazi wa Wilaya ya Mafinga mkoani Iringa.
Wamefikishwa mahakamani leo Jumanne Februari 25, 2020 na kusomewa shtaka moja la kutoa rushwa.
Baada ya kusomewa shtaka lao, walikiri kutenda kosa hilo na
Hakimu Shaidi amesema kesi hiyo itaendelea kesho kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 26, 2020 itakapoendelea na washtakiwa wamerudishwa rumande.
==>>Msikilize Hapo Chini
_______________==>>Msikilize Hapo Chini
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment