Serikali imesema imeanza mchakato wa kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Uingereza dhidi ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).
ATCL imeamriwa kulipa Dola 30.1 milioni (Sh69.23bilioni) kwa kampuni moja ya Liberia kama fidia baada ya kuvunjika kwa mkataba wa kukodisha ndege.
Kesi hiyo inahusu makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2013 na aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka ya kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kampuni ya Willis Trading.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Uingereza, Christopher Butcher aliiamuru ATCL kulipa fedha hizo pamoja na riba inayoweza kufikia dola 10 milioni (Sh23 bilioni) kwa kampuni hiyo ya Liberia, ambayo inajishughulisha na masuala ya kuuza na kukodisha ndege, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi amesema kuwa mkataba wenyewe ulikuwa wa kifisadi wa kuitia nchi hasara.
Dk Kilangi alisema kuwa serikali imewasiliana na ofisi yake, ambayo imeanza mchakato wa kukata rufaa.
“Tumeanza mchakato wa kukata rufaa na tunazingatia sheria na taratibu za Uingereza,” aliongeza.
“Tumeanza mchakato wa kukata rufaa na tunazingatia sheria na taratibu za Uingereza,” aliongeza.
Dk Kilangi alieleza kuwa hukumu hiyo imewashangaza kutokana na ukweli kuwa ndege yenyewe ilitumika kwa miezi saba tu.
“Hawa watu wameibia nchi na tutapambana mahakamani kuhakikisha tunashinda kesi hii,” alisisitiza Kilangi.
Credit: Mwananchi
“Hawa watu wameibia nchi na tutapambana mahakamani kuhakikisha tunashinda kesi hii,” alisisitiza Kilangi.
Credit: Mwananchi
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment