Ebitoke Kushiriki Miss Tanzania 2020

Mchekeshaji Annastazia Exavery (22) maarufu Ebitoke amesema atashiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2020.

Akizungumza leo Ijumaa Februari 28, 2020 Ebitoke ametaja sababu tatu za kushiriki shindano hilo, “sababu ya kwanza mimi ni mrembo nisingependa kutumia urembo huu kwa mambo mengine yasiyokuwa na tija, ndio maana nimeamua kushiriki kwa kuwa kuna fursa nyingi.”

“Pili nataka kuwaonyesha vijana kuwa hakuna kinachoshindikana kama mtu ukiamua, hii itasaidia wengi kujiamini na kushiriki. 

"Tatu, mimi ni msanii napaswa kubadilika. Katika urembo ni moja  ya njia kuonyesha kipaji changu kingine mbali ya kuigiza filamu na vichekesho.”

Mwandaaji  wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi amethibitisha ushiriki wa Ebitoke akibainisha kuwa amerudisha fomu jana.

Ebitoke amewashuruku mashabiki wake kwa kuendelea kuwa naye kwenye sanaa ya maigizo ila kwa sasa ameamua kujitosa kwenye kinyanganyiro hicho kwa kuanzia Kanda ya Ziwa akiwakilisha mkoa wa Kagera.

“Napenda kuwajulisha rasmi tayari nimesha jaza form ya kushiriki Miss Tanzania kanda ya Ziwa 2020 nikiuwakilisha mkoa wangu wa Kagera na nimeiwasilisha kwa wahusika. Ni imani yangu nitafika mbali, nahitaji support yenu,” amesema Ebitoke. 


from MPEKUZI

Comments