Mbunge Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amemjibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyehoji sababu za yeye kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania inyimwe mkopo wa elimu..
Ndugai ametoa kauli hiyo leo Ijumaa bungeni ambapo amesema Zitto kuandika barua hiyo ni tofauti za kisera, lakini kuzuia fedha za Benki ya Dunia ni kwenda mbali zaidi na haimsaidii chochote zaidi ya kuwakomoa wananchi Wanyonge.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Zitto ambaye yupo nchini Uingereza amesema, “hakuna tofauti ya kisera katika suala la watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Ilani ya CCM iliahidi hilo, wananchi mwaka 2015, vyama vya Upinzani viliahidi hilo na wananchi 2/3 wanaunga mkono hilo.”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment