Jumatatu, Januari 27, Rais Uhuru alifanya mkutano na naibu wake William Ruto katika Ikulu, jijini Nairobi na kumuelezea mikutano tofauti ya BBI inayopangwa na wandani wa Ruto.
Huku akimsomea Ruto hatia ya ghasia, Kiongozi wa Taifa alisema hakuridhishwa na mipango ya wapinzani wake kutaka kusambaratisha juhudi zake kuwaunganisha Wakenya kupitia BBI ambayo ni matunda ya handisheki ya mwezi Machi 9, 2018.
Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu mnamo Jumanne, Januari 29, aliwaduwaza Maseneta baada ya kuonekana kumkana Susan Wangari Ndung'u kuwa mkewe. Waititu na mke wake Wangari walituhumiwa na ufisadi na walitolewa madarakani na bunge la kaunti lake
Mwanamume mmoja kutoka kaunti ya Busia amewaomba polisi kumsaidia kumtafuta mwanawe ambaye anaripotiwa kuuzwa KSh 18,000 na mke wake. Benard Ojiambo Oduori anaamini kuwa mke wake alimuuzia dada yake mtoto huyo ambaye ni tasa jijini Nairobi mnamo Desemba mwaka jana wakati malaika huyo alikuwa na wiki mbili.
Wanasiasa kutoka Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, wamedai kuwa wabunge wa mrengo wa Tangatanga wamebuni njama ya kumwondoa Rais Uhuru Kenyatta madarakani. Kikosi hicho cha Raila kilisema Ruto aliwaagiza wandani wake kuanza kukusanya saini ili kuwasilisha mswada huo bungeni.
Hatma ya Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu itaamuliwa hii leo na maseneta ambao wataunga mkono ama kupinga uamuzi wa madiwani.
-TukoKenya
-TukoKenya
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment