Uingereza imeondoka rasmi katika Umoja wa Ulaya saa sita usiku tarehe 31 Januari 2020 kwa saa za Brussels, Ubelgiji kwa mujibu wa makubaliano, na imekuwa ni nchi ya kwanza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya katika historia ya umoja huo.
Mchakato wa kujitoa kwenye umoja huo uliodumu kwa miaka mitatu na nusu umekamilika jana, ambapo pia utakuwa ni mwanzo wa uhusiano wa aina mpya kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya katika siku za mbele.
Baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itakuwa na kipindi cha mpito cha miezi 11 hadi tarehe 31 Desemba 2020. Katika kipindi hicho, pande hizo mbili zitafanya mazungumzo kuhusu uhusiano baina yao, ambapo ajenda kubwa itakuwa ni kufikia makubaliano ya biashara huria.
Hata hivyo muda wa miezi 11 ni mfupi kuweza kukamilisha mazungumzo hayo, na matokeo yake yatajulikana baadaye. Uingereza ilijiunga kama mwanachama mwaka 1973.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment