Spika Ndugai Asema Wanamsubiri Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa benki ya dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini

Spika wa Bunge, Job Ndugai Leo Ijumaa Januari 31, 2020 amesema wanamsubiri Mbunge Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa benki ya dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini 

Fedha za mkopo huo ambazo ni zaidi ya Sh1.2 Trilioni zingeelekezwa katika programu za shughuli za elimu.

Kikao hicho kilipangwa kufanyika Jumanne Januari 28, 2020  kwa ajili ya kuidhinisha mkopo huo, lakini kikaahirishwa dakika za mwisho kutokana na kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya nje kuwa ni ombi la taasisi ya kijamii ambayo ina wanachama wake Tanzania.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”


from MPEKUZI

Comments