PICHA: Maspika Wastaafu wa Bunge Wakabidhiwa Majoho Yao Waliyokuwa Wakiyatumia

Bunge limeamua kuwapa heshima maspika wastaafu kwa kuwakabidhi majoho waliyokuwa wakiyatumia.

Shughuli hiyo ya kukabidhi majoho imefanyika leo katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18 wa Bunge.

Joho la Spika wa Bunge la tisa marehemu Samuel Sitta limepokelewa na mkewe Margaret Sitta ambaye ni mbunge wa Urambo (CCM).

Margaret ameungana na maspika wastaafu, Pius Msekwa na Anne Makinda kupokea majoho waliyoyatumia wakati wakiongoza chombo hicho cha Dola kwa nyakati tofauti.


from MPEKUZI

Comments