Maalim Seif Kuchukua Fomu Ya Kugombea Nafasi Ya Uongozi Katika Chama Cha ACT- Wazalendo

Kama inavyofahamika, Chama cha ACT Wazalendo tayari kimetangaza rasmi kuanza kwa Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa ndani ya Chama baada ya kukamilika chaguzi katika ngazi za chini. 

Shughuli ya kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi mbali mbali za uongozi katika ngazi ya Taifa imetangazwa kufanyika kuanzia tarehe 27 Januari hadi 26 Februari, 2020.

Kwa taarifa hii, tunawajulisha kuwa leo siku ya Alkhamis, tarehe 30/01/2020 saa 5.00 asubuhi Maalim Seif Sharif Hamad anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi mojawapo kati ya nafasi za uongozi zilizotangazwa kugombewa katika Chama Cha ACT Wazalendo. Shughuli hiyo itafanyika Ofisi Ndogo ya Chama iliyopo Vuga, Zanzibar.

Kwa taarifa hii, ndugu waandishi wa habari mnaalikwa rasmi kushuhudia tukio hilo la uchukuaji wa fomu.

 Maalim Seif pia anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu dira na mwelekeo wake juu ya nafasi ya uongozi anayokusudia kuiomba katika Chama.

Nyote mnakaribishwa.

Imetolewa na;
Ofisi ya Maalim Seif Sharif Hamad
30/01/2020


from MPEKUZI

Comments