Jeshi la Polisi Dodoma Lanasa Komputa Yenya Miradi ya Umeme wa Tanzania ,Kenya na Zambia Iliyoibiwa na Mlinzi

Jeshi la Polisi Mkoa wa  Dodoma limemkamata  Boniface  Mushi  ambaye ni mlinzi  wa Ofisi za TANESCO  baaada  ya kuvunja ofisi za hizo eneo la area D jijini Dodoma   na kuiba kompyuta mpakato[Laptop].

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jan,27,2020 jijini
Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoani hapa Girres Muroto   amesema msako mkubwa  ulifanyika katika eneo hilo  ambapo mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi  QSS   Deus Mushi  alikamatwa katika eneo la wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza  baada ya kuiba laptop hiyo kutoka Dodoma  katika
ofisi za TANESCO,  za mradi wa miundombinu  ya umeme  shirikishi ya nchi tatu  ambazo ni Tanzania ,Kenya na Zambia.

Katika tukio jingine kamanda Muroto amesema  katika Mtaa wa Kizota jijini Dodoma  alikamatwa Joshua Elisha [38] mlinzi wa Kampuni ya ulinzi ya KK Security  mkazi wa     Kizota Mbuyuni  akiwa na Compresssor ya  friji kubwa ambayo ni mali ya wizi  aliyoiba baada ya kuvunja  store ya lindo .

Aidha,Kamanda Muroto amesema  jeshi hilo limeokota Jumla ya pikipiki nne katika maeneo tofauti   zikiwa zimetelekezwa na wahalifu wakati wa doria  ambapo wenye pikipiki walikimbia baada ya kukurupushwa  wakiwa kwenye harakati za kufanya uhalifu na pikipiki hizo ni MC.813 CDH Fekon nyekundu MC .128 CCQ BOXER nyekundu  MC 857 CCU TVS nyekundu  naT. 967  CKK  BOXER  nyeusi ambapo imebainika kuwa ni Namba bandia.

Pia,Jeshi hilo limefanikiwa kukamata nyara za serikali  huku likiwaasa wananchi  kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu mbalimbali nchini wakiwemo waendesha bodaboda nyakati za usiku.


from MPEKUZI

Comments