Rais Uhuru Kenyatta amesema wakili aliyetimuliwa nchini Kenya Miguna Miguna yuko huru kurejea Kenya kwani ni haki yake Kikatiba.
Kiongozi huyo wa taifa alisema Miguna ataruhusiwa kurejea nchini lakini atumie uhuru wake wa kujieleza kueneza amani na umoja miongoni mwa Wakenya.
Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Charles Rubia katika Kaunti ya Murang’a mnamo Jumatatu, Desemba 30, Uhuru alisema serikali yake itatoa uhuru kwa Wakenya wote kama ilivyopiganiwa na viongozi waliotangulia.
“Hakuna mtu ambaye amezuiwa kusema yale anayotaka kusema. Ata nasikia kuna wengine wanataka kupanda ndege warudi..waendelee..hio ni uhuru wao," alisema kiongozi huyo wa chama cha Jubilee.
Wakili Miguna anatazamiwa kuingia nchini Jumanne 7, Januari 2020.
Wakili huyo alitangaza kuwa atarejea nyumbani kupitia ukurasa zake za utandawazi siku ya Alhamisi, Desemba 19.
“Narejea nyumbani. Haki ya kuzaliwa, Haki ya Katiba na amri ya korti. Mabadiliko kwa ushawishi. Nitawasili: Jumanne, Januari 7, 2020 mwendo wa saa tatu na dakika 25 usiku kupitia ndege ya Lufthansa LH 590,” aliandika Miguna kwenye Twitter.
Wakili huyo alitimuliwa Kenya kwa mara ya kwanza Februari 2018 baada ya kumuapisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kama rais wa watu mnamo Jumanne, Januari 30 katika bustani ya Uhuru.
Mnamo Machi 2018, juhudi zake za kuingia nchini ziliambulia patupu huku serikali ikisema kwamba aliasi uraia wake wa Kenya ili kuwa raia wa Canada.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment