Mwanamke aitwae Mary Richard Mushi wa Kilinga Arumeru Arusha ameuawa kwa kukatwa na shoka na Mtu anayedaiwa kuwa Mume wake Moses Pallangyo aliyekuwa akiishi naye ambae ni Mwimbaji wa nyimbo za injili .
Akizungumza jana katika Kijiji cha Kilinga wilayani humo, baada ya kutembelea kuona mauaji hayo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro, alisema alifika muda mchache eneo la tukio baada ya tukio hilo kutokea.
"Kweli nimesikitishwa sana na tukio hili lililotokea siku ya Sikukuu ya Krismasi nawapa pole wananchi wa kijiji hiki kwa tukio hili baya lililoharibu sikukuu yetu," alisema.
Kwa mujibu wa Muro, tayari vyombo vya dola vimeanza msako mkali kumtafuta mtuhumiwa ili atiwe mbaroni.
"Nawaomba wananchi muwe watulivu na mtuachie vyombo vya usalama tulifanyie kazi na wananchi wanaofahamu mahali alipokimbilia mtuhumiwa wasaidie vyombo vya dola kuvipa taarifa," alisema.
Baba mzazi wa mtuhumiwa, Latiaeli Pallangyo, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu majira ya mchana.
Alisema Marry (marehemu) na mwanawe Mosses wana wiki tatu tangu tangu waanze kuishi pamoja kama mume na mke.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment