Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Njombe,kimetoa wito kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajia kuanza disemba 30,2019 mpaka januari 5,2020 mkoani humo.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Rose Mayemba wakati akizungumza na vyombo vya habari.
“Tunafahamu kwamba wananchi wamekatishwa tamaa sana na zoezi lililopita kwenye serikali za mitaa,wengi ile hari imekufa, lakini nitoe rai kwa wananchi wasiache wajibu wao wa kwenda kujiandikisha” alisema Rose Mayemba

Mwenyekiti Rose Mayemba amewaagiza viongozi wa chama hicho kuto kuacha kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha mara baada zoezi hilo kukamilika katika maeneo mengine ya nchi na sasa zoezi hilo linatarajia kuanza mkoani humo.
Aidha amesema kama vilivyowekwa vipaumbele vya chama hicho ikiwemo kudai tume huru ya uchaguzi,chama hicho hakitaweza kwenda kwenye uchaguzi bila ya kuwa na tume huru.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment