BREAKING NEWS : Sumaye aondoka Rasmi CHADEMA

Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye leo Desemba 4, 2019 ametangaza kuondoka CHADEMA.

Akiongea leo kwenye mkutanao wake na waandishi wa Habari, Sumaye amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na figisu alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kua nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi.


==>>Hapo chini kuna nukuu ya mambo aliyayasema leo;


"Lile tangazo lililotoka jana, ilikuwa ni kweli kutoka kwenye Ofisi yangu lakini halikutengenezwa kwa lengo lile kwa hiyo naomba mliache kama lilivyo.
 
"Najua kuna mambo mengi yameandikwa juu ya kikao hichi kwa watu ambao wanajifanya wapiga ramli, ila naomba muyapuuze, ila yakweli ni haya nitakayoongea

"Kanda ya Pwani nilipata habari kuna watu walinifuata nigombee Uenyekiti Kanda, nongwa ilikuja baada ya mimi kuamua kugombea Uenyekiti Taifa, ila lengo la kwanza nilitaka kuondoa hisia kuwa ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia ya kweli


"Niliwaambia wajumbe kuwa mkifanya kama mlivyotaka kufanya, nitauthitibitishia umma kuwa ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia ya kweli, au kiti cha Mbowe kina utaratibu mwingine.

“Nafasi ya Mwenyekiti Mbowe haiguswi mimi nilitaka kuonesha kuwa hilo sio kweli lakini nilikuwa najidanganya nimefanyiwa figisu kwenye uchaguzi wa kanda kisa niligusa kiti cha Uenyekiti Taifa

“Mbowe aliwahi kutupa nasaha kuwa tusiionje sumu kwa kuilamba, na mimi siwezi kuigusa sumu kwa kuilamba leo natangaza rasmi kuwa sitoendelea kugombea kwenye nafasi ya Uenyekiti Taifa CHADEMA.

“Nimefedheheka sana kwa kitendo kilichofanywa hasa kwa kujua nimefanyiwa hivi kwasababu ya kukigusa kiti cha Uenyekiti Taifa.

“Kama wakubwa wameamua kuwashawishi wapiga kura wangu wa Kanda ya Pwani hata kwa kuwaficha Hotelini, hii maana yake naambiwa Sumaye akufukuzae akuambii toka.

"Baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote

“Najua katika kujikosha yatakuwepo maneno Kama kapewa fedha na CCM au ACT n.k, kama nilipokuja CHADEMA nilipewa pesa basi na safari hii nimepewa fedha ingawa sijui na nani maana sijiungi na Chama chochote

“Na kama nilikuja CHADEMA kwa hiari yangu bila kupewa pesa basi na safari hii sijapewa pesa na sitopewa pesa maana sijiungi na Chama chochote, mimi sijawahi kuwa Kibaraka wa Mtu wala Kikundi na hata siku moja sito kuwa hivyo


from MPEKUZI

Comments