Jumia Yafunga Biashara zake Tanzania

Mtandao wa biashara Barani Afrika umefunga biashara yake nchini Tanzani ikiwa ni siku chache tu baada ya kusitisha shughuli zake nchini Cameroon

Kulingana na taarifa iliyopatikana imeeleza kuwa Jumia imefunga shughuli zake nchini Tanzania ili kuwekeza rasilimali katika masoko mengine

Taarifa hiyo inasomeka:
"Kwa kuzingatia tathmini yetu ya kuelekea mafanikio, tumefanya maamuzi magumu ya kusitisha shughuli zetu  Tanzania kuanzia Novemba 27, 2019.

"Tanzania kuna fursa kubwa lakini tumeona ni vyema kutumia rasilimali zetu katika masoko mengine, uamuzi huo sio rahisi lakini unatusaidia kuweka mkazo na rasilimali zetu mahali ambapo tunaweza  kuleta matunda na kusaidia ustawi wa Jumia"

Aidha, imesema itaendelea kutumia mtandao wake wa ''Jumia Deals'' katika kuendelea kuwasaidia maelfu ya wafanyabiashara ambao wanautumia kukutana na wanunuzi

Novemba 18, 2019 kampuni hiyo ambayo makao makuu yake yapo nchini Nigeria ilifunga biashara zake  nchini Cameroon kwa sababu kama hizo.


from MPEKUZI

Comments