Tatizo la Uhaba wa vitabu kwa wanafunzi katika shule za msingi katika Halmashauri ya Mji Kahama kuwa historia
Katika Jitihada za kukabiliana na uhaba wa vitabu vya Masomo ya sayansi na hisabati katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinayanga Idara ya elimu Msingi imegawa vitabu elfu 88,652 vya darasa la awali hadi darasa la tano katika shule za msingi 72 zilizopo Halmashauri hiyo ili kukuza kiwango cha taaluma.
Hayo yamebainishwa jana na Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu Mwalimu Sadick Juma,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa Vitabu hivyo ni vya masomo ya Hesabu, Kiswahili, kingereza, Sayansi, Uraia na Maadili, Maarifa ya jamii ambavyo ni maalumu kwa wanafunzi wa darasa la awali hadi tano.
Amesema hapo awali kulikuwa na tatizo la uhaba wa vitabu ambapo wanafunzi watatu walikuwa wanatumia kitabu kimoja hivyo upatikanaji wa vitabu hivyo utakuwa suluhisho kwani kwa sasa kila mwananfunzi atakuwa anatumia kitabu chake mwenyewe.
Vitabu hivyo vimegawanyika katika makundi yafuatayo Kiswahili darasa la tatu vitabu 2676,kusoma darasa la kwanza 4133,kuhesabu darasa la kwanza 4133,sayansi darasa la tatu 2676,hisabati darasa la tatu 2676,kiingeza darasa la tano 300.
Kiswahili darasa la nne 2739,uraia na maadili darasa la nne 2672,maarifa ya jamii darasa la tatu 114,hadithi darasa la awali 24,kifaransa hatua ya kwanza kwa darasa la kwanza hadi la tatu 277 na darasa la nne hadi la saba 277, na hisabati darasa la tatu 376
Amefafanua kuwa mbali na kugawa vitabu hivyo kwa wanafunzi wa darasa la awali hadi latano, pia Halamshauri hiyo inatarajia kupokea vitabu vingine kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la sita na la saba huku asilimia kubwa ya vitabu hivyo vikiwa vya masomo y sanyansi na hisabati.
Katika Hatua nyingine Mwalimu Juma Hata amesema kuwa, mbali nakutoa vitambu hivyo bado wanakabiliwa na uhaba wa walimu katika shule za msingi ambapo mwaka jana wa 2018 Halmashauri ya mji wa kahama ilipokea walimu 20 wapya ambapo wanauhitaji wa walimu zaidi ya 600.
Mwalimu Juma alitolea mfano Shule ya msingi Mhungula inawanafunzi 4000uhitaji wawalimu 88 na walipo 39, na Shule ya Msingi majengo inajumla ya wanafunzi 2800 na inauhitaji wa walimu 64 na walipo ni 36 laki shule hizi zimeonekana kufanya vizuri katika mtihani mbalimbali ya kitaifa.
Amesema Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu ,shule tatu kati ya shule za msingi 72 za serikali zilizopo Halmashauri ya mji wakahama zimefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba ambazo ni shule ya msingi Kinaga iliyoshika nafasi ya kwanza katika Halmasghauri hiyo,Kilima B, Majengo pamoja na Kahama B,na shule zilizofanya vibaya ni shule ya msingi Bukooba, Mpera, Bujika na Shule ya msingi Nyandekwa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment