Taarifa Kwa Umma: Tahadhari Juu ya Matapeli Wanaotumia Jina la Askofu Mkuu Ruwa'ichi Kutapeli Watu

Katibu  Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Frank Mtavangu, ametoa tahadhari ya kuwepo kwa ukurasa wa facebook bandia ambao unatumiwa na matapeli kuomba fedha huku wakitumia jina la Askofu Mkuu wa jimbo hilo Yuda Rwai’chi.

Taarifa iliyotolewa na katibu huyo jana jijini Dar es Salaam ilisema matapeli hao wamekuwa wakidai kuwa wanaomba mchango kwaajili ya ujenzi wa makazi ya malezi ya wajane, yatima na wakongwe.

“Napenda kuwatahadharisha kuwa kuna matapeli wamefungua akaunti ya Facebook kwa jina la Askofu Mkuu Yuda Thadei Rwai’chi akaunti hii ni ya kitapeli inayotumia jina la “Askofu Ruwai Chi”.

“Inaomba watu wachangie ujenzi wa makazi kuu ya malezi ya wajane, yatima na vikongwe ikiomba michango itumwe kwenye namba ya simu,”alieleza Mtavangu.

Alisema Askofu hatumii akaunti hiyo na hajawahi kuomba michango ya namna hiyo kwa njia hii na akaunti hiyo sio yake .


from MPEKUZI

Comments