Saudi Arabia yasitisha shughuli katika vituo vya mafuta vilivyoshambuliwa na Waasi wa Yeman

Saudi Arabia imesitisha kwa muda uchimbaji mafuta katika vituo viwili ambavyo vimeshambuliwa na ambavyo vinamilikiwa na kampuni ya mafuta ya nchi hiyo Saudi Aramco.

 Waziri wa nishati ambaye pia ni mwanamfalme Abdulaziz bin Salman amesema hayo jana kupitia taarifa, na kuongeza kuwa kufuatia mashambulizi hayo, uchimbaji mafuta katika vituo hivyo umepungua kwa asilimia 50. 

Waasi wa Houthi wenye mafungamano na Iran wamethibitisha juu ya kurusha ndege 10 zisizokuwa na rubani zilizoshambulia vituo hivyo vya mafuta. 

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani  ya Saudi Arabia, hujuma hizo zimesababisha moto katika vituo hivyo. 

Msemaji wa wanamgambo wa Yemen amesema shambulio hilo "ni jibu" kwa operesheni za kijeshi zinazoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Wahouthi nchini Yemen. 

Marekani imeituhumu Iran kwa kuhusika na mashambulizi hayo.


from MPEKUZI

Comments