Iran yakataa kufanya mazungumzo na Marekani hadi Iondolewe Vikwazo

Rais wa Iran hapo jana ameondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo na Rais Donald Trump, licha ya juhudi za dakika za mwisho za viongozi wa mataifa ya Ulaya wanaotaka kupunguza mvutano huku Marekani ikiongeza tena vikwazo vya adhabu dhidi ya Iran. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa siku mbili bila ya mafanikio amekuwa akijaribu kuwakutanisha viongozi hao wawili wakiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Macron anajaribu kufanikisha mkutano huo wa kihistoria ambao anatumai utaepusha kutokea vita katika Mashariki Kati. 

Lakini Rais wa Iran Hassan Rouhani, akihutubia katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa amesema hatokubali kufanya mazungumzo wakati Marekani inaendelea kuiwekea vikwazo nchi yake.


from MPEKUZI

Comments