Hatimaye Benjamin Netanyahu achaguliwa kuunda serikali mpya Israel

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hapo jana usiku amepewa jukumu na Rais wa Israeli Reuven Rivlin la kuunda serikali mpya, kufuatia uchaguzi uliosababisha mkwamo wa kisiasa. 

Rais Rivlin amechukua uamuzi huo baada ya juhudi za kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kati ya chama cha Netanyahu cha Likud na chama cha Bluu na Nyeupe cha mpinzani wake Benny Gantz kushindikana. 

Rais ana jukumu la kikatiba la kumteua waziri mkuu baada ya uchaguzi wa kitaifa. Netanyahu anazo siku 28 za kuunda serikali mpya, na anaweza kuomba kuongezwa wiki mbili. 

Netanyahu akishindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha ili awe na wingi wa viti bungeni, Gantz badala yake atapewa nafasi ya kuunda serikali ya mseto.


from MPEKUZI

Comments