Gunia 515 Za Kahawa Ya Magendo Zakamatwa Mkoani Kagera Zikisafirishwa Kwenda Nchi Jilani Ya Uganda.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limekamata magendo ya kahawa katika kata ya Kemondo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kituo cha polisi Bukoba mkoani Kagera  SSP Babusanare wakati akiongea na waandishi wa habari  na kusema kwamba mnamo tarehe 24 Septemba  mwaka huu askari waliokuwa doria walipata taharifa kuwa gari lenye usajili NO.T.205 DHX Mitsubishi Fuso lilikamatwa kwa kosa la kusafirisha kahawa bila kibali.

Ameongeza kuwa magendo hayo yalikamatwa  katika maeneo ya Bulila, Kata Kemondo, Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ambapo yalikuwa yanapitia Mwalo wa Bilolo kemondo kuelekea nchini Uganda.

Bwana Babusanare amesema kuwa gari hilo lilikuwa na kahawa gunia 515 na kila gunia lina kilo 70  na kuongeza kuwa dereva wa gari iyo alitokomea kusiko julikana baada ya kuona anakamatwa na polisi na kuongeza kwamba jitihada za kumtafuta dereva huyo bado zinaendelea  na kusema kwamba watuhumiwa wote wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi wilaya ya Bukoba kwa mahojianio zaidi.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Sadick Charles, Jonizius Gerad na Lazaro Mdesa.

Kwa upande wake Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba DC Deodatus Kinawilo amepongeza juhudi za jeshi la polisi kukamata gari hilo na kuhakikisha kila aliyehusika katika kusafirishwa kwa magendo hayo ya kahawa sheria inafuata mkondo wake na kuwawajibisha ipasavyo.

“Dolia hii iwe endelevu hasa katika maeneo mnayoyadhania yanaweza kuwa na makosa ili kutetea juhudi za Rais wetu Mh.Dk.John Pombe Magufuli kutokana na makosa yanayojitokeza katika kahawa maana watu kama hawa wanarudisha maendeleo nyuma hawatakiwi kuachwa kabisa” Alisema Kinawilo.


from MPEKUZI

Comments