Askari wawili JWTZ Wafariki kwa Ajali....20 Wajeruhiwa

Askari 2 wa JWTZ kikosi cha 24 KJ Kigoma,wamefariki na 20 kujeruhiwa katika  ajali iliyotokea Mkoani Katavi baada ya gari la jeshi lililokuwa limebeba askari kupinduka eneo la Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kigoma Maweni, Lameck Mdengo amethibitisha vifo hivyo na kupokea majeruhi hao na kuwataja waliofariki ni Bakari Mohammed (38) na Rashid Mwimbe (28).

Majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.


from MPEKUZI

Comments