Waziri Mahiga Akutana Na Viongozi Mbalimbali Jijini Dodoma Katika Mkutano Wa Mfumo Wa Maborsho Ya Sheria Ya Haki Za Jinai.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh Augustine Mahiga leo amekutana na Viongozi mbalimbali Jijini Dodoma katika Ufunguzi wa Mkutano wa kuhitimisha Mfumo wa maboresho ya Sekta Ndogo ya Mfumo wa Sheria ya Haki za Jinai.
 
Katika mkutano huo Dkt Mahiga amesema kuwa mara ya mwisho kupitia Mfumo huo na kuufanyia Marekebisho ni takribani Miaka Ishirini iliyopita, toka wakati huo mambo mengi yamebadilika na Uhalifu umekuwa na Mbinu tofauti hivyo ni muhimu kupitia Mfumo huo ili kuendana na wakati uliopo.
 
Ameongeza kuwa maboresho hayo yanahusisha Mnyororo wa hatua mbalimbali zinazotokea wakati wa kushugulikia Uhalifu kuanzia Ngazi ya kuzuia uhali usitokee, kutambua unapokea, kukakamata wanaofanya uhalifu na kadhalika.
 
Akielezea mlolongo mzima ulivyoshirikisha aina mbalimbali za ngazi za Uongozi, katika kupitia Madhaifu na Maboresho, Naibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Anastazi Mpanju amesema kuwa baada ya hapo Wizara itakuja na mpango Mkakati wa Kitaifa wa Miaka Mitano katika kutatua Changamoto zilizopo.
 
Sambamba na hayo Dkt Mahiga amepongeza wote walifanikisha mchakato huo kwa ushirikiano wa serikali na wadau wa wao wa maendeleo, shirika la maendeleo la watu wa uingereza DfiD kwa mchango walioonesha kusaidia jitihada za nchi yetu katika maboresho ya mfumo wa haki.


from MPEKUZI

Comments