Wananchi Mkoani Kagera Watakiwa Kuacha Tabia Za Kuwahifadhi Wahamiaji Haramu.

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI,KAGERA.
Mkuu wa wilaya ya Missenyi  Mkoani Kagera Kanali Denice Mwila  amewataka wananchi wilayani missenyi kuacha tabia za kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji haramu kutoka nchi jirani jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa nchi.
 
Kanali MWILA ametoa kauli hiyo na kusema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikipelekea wahamiaji haramu kuongezeka wilayani missenyi mkoani hapa  hivyo kupelekea watanzania kukosa ardhi ya kulima na kufanya shughuli za ufugaji.
 
Kutokana na hali hiyo,kanali MWILA amesema kuwa watanzania katika maeneo ya mipakani hususani kata za Mtukula,Kakunyu na Minziro wanatakiwa kuhakikisha wanaepuka kupokea rushwa kutoka kwa wahamiaji ili wawape hifadhi.
 
Amesema kuwa serikali wilayani humo haitawafumbia macho wananchi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.


from MPEKUZI

Comments