Na Mwandishi wetu- MAELEZO
Serikali yawahakikishia wamiliki wa Viwanda nchini kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayoimarisha ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuweka mipango mahususi ya kuongeza uzalishaji ili kuendana na mahitaji ya Masoko katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza na wamailiki hao leo Julai 28, 2019 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amesema kuwa wamiliki hao wanapaswa kuendelea kukuza uwezo wa uzalishaji bidhaa ili kuendana na soko lililopo katika jumuiya hizo.
“Tunayo kila sababu ya kuhakikisha kuwa Serikali na wamiliki wa Viwanda tunaweka mikakati ya pamoja Ili kuweka mazingira wezeshi yatakayokuza sekta ya viwanda hapa nchini”. Alisisistiza Mhe Bashungwa.
Akifafanua amesema kuwa sekta ya Viwanda inasaidia kuzalisha ajira na kuchangia katika kuwezesha maendeleo endelevu kwa kuimarisha viwanda vilivyopo na vipya kwa maendeleo ya nchi yetu.
Akizungumzia changamoto za sekta hiyo Mhe Bashungwa amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuchukua changamoto za wamiliki wa Viwanda na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka ili dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda itimie kwa wakati kwa maslahi mapana ya Taifa na wamiliki wa viwanda hivyo.
“Serikali ya Awamu ya Tano na Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli inatoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa dhana ya ujenzi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo kwa kujenga mazingira wezeshi katika sekta hii muhimu kwa ujenzi wa viwanda” Alisisitiza Mhe. Bashungwa.
Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Bashungwa umelenga kuimarisha sekta ya viwanda hapa nchini kwa kuweka mikakakati itakayowawezesha kumudu ushindani wa bidhaa kutoka za nje.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment