Spika Mstaafu Anne Makinda Atoa Ushauri kwa Madiwani Wanawake

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amewataka wabunge na Mdiwani wa vitimaalum nchini kusimamia kikamilifu rasilimali za umma ili ziwanufaishe wananchi wote.

Akizungumza Jijini Mwanza katika semina ya kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wa serikali za Mitaa (WASEMI) iliyoandaliwa na shirika la TGNP Mtandao, Makinda alisema kwamba, mchango wa wabunge na madiwani wa viti maalum umekuwa hauonekani vizuri au kutambuliwa na jamii kutokana na wao wenyewe kuwa na hofu au kutokujiamini kitu ambacho kimechangia kuwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea mbele.

“Tatizo letu sisi viongozi Wanawake, tunajenga hofu, tunaogopa sana kujitokeza na kuwajibika vizuri kwa wananchi, eti kwa sababu ni viti maalum. Sisi tulianzia pia viti maalum , lakini tulipata nafasi ya kwenda jimboni kwasababu tulijiamini, tuliwajibika kikamilifu na tulihangakikisha uwezo wetu unaonekana na kila mmoja. Jitokeze, kwa wananchi, watumikie kwa uadilifu na watakuona na kutambua mchango wako” alisema Makinda

Makinda amewaasa wanawake viongozi wa serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma za jamii kwenye halmashauri zao na kuhakikisha kila kinachofanyika kwenye halmashauri wanakielewa vizuri na kutoa taarifa kwa wananchi wote.


from MPEKUZI

Comments