RC Telack Aingilia Kati Sakata la kumkataa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga

NA SALVATORY NTANDU
Serikali mkoani Shinyanga imesema Uamuzi uliochukiliwa na  Madiwani  wa manispaa ya Shinyanga ya kumkataa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Geofrey Mwangulumbi kuwa ni batili kwa kuwa haukuzingatia sheria.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, wakati akizungumza na Madiwani hao na kuwataka kutengua uamuzi huo ili kuruhusu shughuli za serikali kuendelea,

Amesema kuwa Madiwani hao  walipaswa kupeleka malalamiko hayo katika ofisi yake  ili yafanyiwe kazi, pamoja na kuitisha baraza maalumu ambalo maazimio yake yangekuwa na ajenda hiyo lakini alishaghaa kusikia tu kikao cha baraza la madiwani kimevunjika madiwani wakimkataa mkurugenzi kutokuwa na imani naye.

Baada ya  kupokea maagizo hayo ya serikali  madiwani hao walikubali kutengua uamuzi huo wa kutokuwa na imani  na mkurugenzi  Mwangulubi na kuendelea na kikao hicho cha  baraza   baada ya jana  kuvunjika.

Mbali ha hilo Telack amewataka madiwani hao kuacha  na malumbano yasiyo na maana kwa kuvunja tu vikao bila ya kufuata taratibu, pale penye mapungufu watoe taarifa ili kuhakikisha manispaa hiyo inapata maendeleo.
 
Amesema tatizo ambalo linasababisha migogoro hiyo kuwepo ni kutoelewana kati ya watumishi wa halmashauri na mkurugenzi wao, sababu kila mtu ni mbabe, na hivyo kusababisha miradi mingi kuwa na usimamizi mbovu na kutotekelezeka, na ndio maana maazimio yenu hayafanyiwi kazi.

Awali Naibu Meya wa manispaa hiyo ya John Kisandu, amesema wametengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi huyo, na kukiri kwamba hawakufuata kanuni na taratibu, hivyo wataendelea kufanya naye kazi, na kumtaka maazimio yao awe ana yafanyia kazi.

Ikumbukwe kuwa juzi  kikao cha baraza hilo la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kilivunjika baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kudai kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri Geofley Mwangulumbi, kwamba amekuwa hatekelezi maazimio ambayo huazimia yakiwamo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


from MPEKUZI

Comments