Ofisa FEKI Wa jeshi la Polisi Atiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linamshikilia Daudi Ramadhani Iddy (23) mkazi wa Tabata Segerea kwa kujifanya ofisa wa Polisi, akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na cheo cha mkaguzi msaidizi wa Polisi( Assistant Inspector).

July 19, 2019 Jeshi la Polisi lilipata tarifa toka kwa askari wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) makao makuu Mlalakuwa, kuwa kuna kijana mmoja amevaa sare za Jeshi la Polisi wana mashaka naye.

Makachero wa Jeshi la Polisi walifika makao makuu ya JKT kumkamata na kufanya naye mahojiano,mtuhumiwa alikiri kujifanya yeye ni afisa wa Polisi na kufanya utapeli.

Pia alikiri kupitia mafunzo Jkt huko Mafinga mwaka 2006 na kujitolea kwa mujibu wa sheria katika kambi hiyo.

Mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi na kupatikana na vifaa vifuatavyo; 
1.Sare moja ya Polisi aina ya kaki 
2. Vyeo vya(Cpl, Sgt na cheo cha mkaguzi msaidizi
 3 Pea moja inaya kombati Jungle green. 
4.Pingu moja. 
5.Kofia moja ya askari wa usalama barabarani. 
6.Radio ya upepo moja aina ya motorola
7 Mikanda miwili ya Jkt.
8.Mkanda mmoja wa bendera wa Jeshi la Polisi, buti na viatu vya kawaida.

Kamanda Mambosasa amesema upelelezi wa kina unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.


from MPEKUZI

Comments