Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu,sera Bunge kazi vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu ,Mhe.Jenista Mhagama ametoa agizo kwa katibu mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha anasimamia na kuwaondoa kazini Maafisa Vijana wanaofanya uzembe wa utekelezaji wa Majukumu yao ndani Ya Halmashauri husika.
Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu,sera Bunge kazi vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu ,Mhe.Jenista Mhagama ametoa agizo kwa katibu mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha anasimamia na kuwaondoa kazini Maafisa Vijana wanaofanya uzembe wa utekelezaji wa Majukumu yao ndani Ya Halmashauri husika.
Mhe.Mhagama ametoa maagizo hayo leo Julai 29,2019 jijini Dodoma Katika uzinduzi wa Mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali na Usimamizi wa biashara kwa vijana .
Mhe.Mhagama amesema pamekuwa na kazi ya mazoea kwa baadhi ya maafisa vijana ngazi ya halmashauri na wamebaki kusubiri fedha za mikopo pekee kutoka serikalini badala ya kuwajibika kutafuta fursa kwa vijana hivyo amesema viongozi wa namna hiyo hawana nafasi kinachotakiwa ni kuwaondoa tu.
Aidha,Mhe.Mhagama ameziagiza taasisi za kifedha hapa hapa nchini kuwa na masharti nafuu ya mikopo kwa vijana kwani sharti la kigezo cha kuweka dhamana ya nyumba kijana hawezi kumudu kwa sababu asilimia kubwa ya vijana wanaishi nyumba za wazazi wao.
Katibu mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji kiuchumi Bi.Beng’i Isa amesema kwa miaka mitano wameweza kuwafikia vijana elfu kupitia program mbalimbali za mafunzo.
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri mkuu,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Bw.Andrew Masawe mafunzo ya kurasimisha ujuzi na mafunzo mtambuka ya kilimo cha kisasa cha kitalu nyumba yamefikia halmashauri 87 hadi sasa huku kila halmashauri ikifikia vijana mia moja [100].
Manaibu mawaziri Ofisi ya Waziri mkuu,kazi,vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Stella Ikupa amesema Programu hiyo itakuwa jumuishi kwa vijana wote wakiwemo wenye ulemavu huku Anthony Mavunde akisema vijana wa kitanzania wanatakiwa kujiamini katika suala la maendeleo.
Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa vijana yanakutanisha kutoka mikoa 26 Tanzania bara huku kaulimbiu ikiwa ni “Wezesha vijana kujiunga na Msingi Endelevu wa ajira”.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment