Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Awataka Wadau Wa Mazingira Kutekeleza Sheria,kanuni,na Taratibu Za Mazingira.
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
MAKAMU wa Rais SAMIAH SULUHU HASSAN amewataka wadau wa mazingira kutekeleza Sheria,Kanuni na maandiko ili kuhimiza utunzaji wa rasilimali misitu na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za maji.
MAKAMU wa Rais SAMIAH SULUHU HASSAN amewataka wadau wa mazingira kutekeleza Sheria,Kanuni na maandiko ili kuhimiza utunzaji wa rasilimali misitu na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za maji.
Akizindua jukwaa la maendeleo endelevu kuhusu usimamizi bora wa misitu kwa upatikanaji wa rasilimali maji endelevu leo jijini Dodoma Makamu wa Rais amesema misitu ndio chanzo kikubwa cha rasilimali maji hivyo isipotunzwa na kusimamiwa vizuri watakuwa wanahatarisha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya kijamii,kibiashara na kuimarisha mazingira.
Ametaja mambo yanayosababisha athari kubwa kwa uhai wa rasiliamli maji kuwa ni kilimo kisichokuwa endelevu,ujenzi holela,uchomaji mkaa,ukataji kuni,uvunaji haramu wa magogo na ufugaji usiozingatia kanuni.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira GEORGE SIMBACHAWENE amesema haridhishwi na hali ya mazingira ilivyo na kuwataka wadau hao kupeleka fedha katika mazingira yanayoharibika badala ya kutumia kwenye makongamano.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta BINILITH MAHENGE amesema ni vyema jamii ikijikita katika kulinda na kutunza mazingira na kwa viongozi kutekeleza yale wanayoazimia.
Naye mkuu wa taasisi ya uongozi profesa JOSEPH SEMBOJA amesema sekta ya maji na misitu ni muhimu hivyo ni vyema sera, mikakati na taasisi zinazohusu sekta hiyo zikafungamana ili ziweze kufnaya kazi kwa ufanisi.
Jukwaa la maendeleo endelevu lilianzishwa mwaka 2012 ili kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji na misitu ili waweze kujadili mpango wa maendeleo endelevu.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment