Korea Kaskazini imesema hivi leo kwamba jaribio lake la makombora mapya linanuia kuwa onyo dhidi ya mipango ya silaha ya Korea Kusini na pia mipango ya kuandaa mazoezi ya kijeshi na Marekani.
Kauli inakuja muda mchache baada ya kombora kurushwa kutoka Korea Kaskazini, ambapo jeshi la Korea Kusini limesema linafanana na kombora la masafa mafupi lililotengezwa Urusi.
Kombora hilo aina ya Iskander lenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia lina uwezo wa kufika popote Korea Kusini, ambako kuna wanajeshi 28,500 wa Marekani, na haliwezi kudunguliwa.
Wachambuzi wa mambo wanasema hatua hii ya Korea Kaskazini ni sehemu ya juhudi zake kuhakikisha inapata kile inachokitaka kwenye mazungumzo yake na Marekani, baada ya mkutano wa hivi karibuni kati ya Kim Jong Un na mwenzake Donald Trump.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment