NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA
Jamii mkoani Kagera imetakiwa kutowabagua wala kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu badala yake wapewe vipaumbele na mahitaji muhimu ili wajione sawa na watu wengine.
Jamii mkoani Kagera imetakiwa kutowabagua wala kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu badala yake wapewe vipaumbele na mahitaji muhimu ili wajione sawa na watu wengine.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa taasisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera Bwana John Joseph wakati akiongea na Mwandishi wa kituo hiki ofisini kwake.
Bwana Joseph amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwatenga, kuwabagua watu wenye walemavu wakiwemo watoto jambo mbalo husababisha makundi hayo kujiona ni watu wa tofauti katika jamii
Amesema katika ushiriki wa makundi ya vijana juu ya mapambano dhidi ya Rushwa Taasisi hiyo imefanikiwa kuyaelisha makundi ya wanafunzi kwa kuanzisha clabs za wapinga rushwa mashuleni
Mkuu huyo amesema ili kulipa uzito suala hilo july 28 mwaka huu wanafunzi wa shule ya Sekondari Kahororo iliyoko mkoani Kagera kwa kushirikiana na Taasisi hiyo watakwenda kutembelea shule ya wanafunzi walemavu katika shule sekondari Mgeza Mseto kwa ajili ya kuwapelekea mahitaji mbali mbali mbali.
Amesema makundi ya watu wenye walemavu ni sehemu ya jamii na ili makundi hayo yatambue kuwa jamii haijawatenga kila mmoja ashiriki katika kuwatembelea kuwajali na kuwapa chochote walemavu waliopo katika maeneo yake.
Hata hivyo ameongeza kuwa jamii iwafichuo na kuwaweka adharani wapate Elimu pamoja na mahitaji yao muhimu.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment