James Mbatia amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi kwa kipindi cha miaka mitano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Jumapili Julai 28, 2019 mkuu wa oganaizesheni na utawala wa chama hicho Florian Mbeo amesema mbali na Mbatia, pia umefanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama chetu ikitokea nafasi mgombea akawa mmoja huwa tunapiga kura za ndio na hapana,” amesema Mbeo akizungumzia uchaguzi huo ambapo nafasi nyingi mgombea alikuwa mmoja.
Amesema nafasi ya mwenyekiti iliwaniwa na Mbatia pekee na kuibuka na ushindi kwa kura 210 za ndio na tisa za hapana.
Mbeo amesema nafasi ya makamu mwenyekiti bara iliwaniwa na Angelina John aliyepata kura 200 za ndio na 19 za hapana.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment