Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa licha ya yeye kuwa mpinzani lakini ataendelea kuipongeza Serikali ya Rais Magufuli.
Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “ACT Wazalendo kimekuwa chama kinachohubiri Ujamaa lakini kwa kuingia huku kwa Maalim Seif ambaye kwenye chama chake cha CUF walikuwa wakitumia mfumo wa Kibepari inabidi tuhamie huko sasa kama tulivyokubaliana na kutakuwa na mabadiliko ya Kiuongozi.“.
“Ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa sana yamefanywa na Serikali hii ya JPM. Japokuwa najua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi.” ameandika Zitto Kabwe na kusisitiza.
“Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu @Nnauye_Nape kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika.” amemaliza Zitto Kabwe.
Hata hivyo, Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa Tweets hizo sio za Zitto Kabwe kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa jeshi la polisi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment