Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Ltd. Mfanyabiashara Rostam Aziz, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuweka usawa wa kibiashara katika miaka minne ya uongozi wake.
Aidha, mfanyabiashara huo ameahidi kuwekeza katika miradi mingine zaidi nchini itakayogharimu zaidi ya Sh bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo.
Rostam amesema hayo leo Jumanne Juni 25, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ghala na mitambo ya gesi ya taifa (Taifa Gas) ambayo ni gesi ya majumbani iliyozinduliwa rasmi na Rais Magufuli.
Anesema mafanikio ambayo wao kama Taifa Gas na makampuni mengine kutoka nje wanayaona yanatokana na kazi kubwa aliyoifanya tangu aingie madarakani mwaka 2015.
“Uimarishwaji wa sekta binafsi utatekelezwa kwa uwanja ulio sawa kama kujenga miundombinu itakayowasaida Watanzania kujikwamua kutoka katika umaskini wa kihistoria na Mheshimiwa Rais historia itakukumbuka katika hili,” amesema Rostam.
“Kuna watu walisema kuwa wewe si rafiki wa sekta binafsi nataka niwaambie kuwa uongozi wako ndiyo umefanya nianze kurudisha mitaji ya uwekezaji ambayo niliwekeza nje, na Taifa Gas ni mwanzo tu ila kuna miradi mingine itakayogharimu Sh bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo,” amesema.
==>>Msikilize hapo chini
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment