Korea Kaskazini Yaitaka Korea Kusini kuacha kuwa mpatanishi katika mazungumzo yao na Marekani

Korea Kaskazini imeitaka Korea Kusini kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mazungumzo yake na Marekani. 

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae In mjini Seoul Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka Japan. 

Moon amesema Korea Kaskazini na Marekani wanatafakari kuandaa mkutano wa kilele kwa mara ya tatu. 

Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim huko Hanoi mwezi Februari uliishia bila makubaliano kuhusiana na Korea Kaskazini kuharibu silaha zake za nyuklia ili ipunguziwe vikwazo. 

Lakini sasa mkurugenzi mkuu katika idara inayohusika na masuala kuhusu Marekani katika Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini Kwon Jong Gun amesema uongozi wa Korea Kusini ni bora ukashughulika na mambo yake ya ndani.


from MPEKUZI

Comments