Bunge laipitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/2020.

Bajeti hiyo ilipitishwa mjini Dodoma  jana baada wabunge kupiga kura ya wazi ya kuitwa mbunge mmoja mmoja.

Matokeo ya kura yalikuwa kama ifuatavyo: Wabunge waliopiga kura walikuwa 380 ambapo 12 hawakuwepo.

Waliosema ‘Ndiyo’ ni 297 sawa na asilimia 78.2 na waliosema ‘Hapana’ ni 83 sawa na asilimia 21.8 .

Hotuba ya Bajeti iliwasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango na mjadala wa bajeti hiyo ulichukua siku saba kabla kuhitimishwa jana.

Awali, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango akijibu baadhi ya hoja za wabunge waliochangia, alisema kamwe saini yake haitoweza kutumika kusaini mikataba, itakayoiuza nchi hata kama atatukanwa vipi.

Alisema ataendelea na msimamo wake huo, ikiwamo kutosaini mikataba mitatu ya miradi mikubwa inayohusu Zanzibar ambayo wafadhili wake wameweka masharti magumu ya dhamana ikiwemo kutaka kutumia mali za jeshi, mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), malikale, mali za kihistoria na za ubalozi kama dhamana ya mkopo.


from MPEKUZI

Comments