Watendaji wa serikali Longido washambuliwa na wafugaji wa mifugo

Na Amiri kilagalila
Mkuu wa wilaya ya Longido Ndugu Frank Mwaisumbe, ameliagiza jeshi la polisi wilayani hapo kuwakamata watu wote walio husika na tukio la kuwapiga watumishi na watendaji wa serikali wakiwa katika utendaji bila kujali vyeo vyao.

Agizo hilo amelitoa jana akiwa katika kijiji cha engarenaibor katika tarafa ya engarenaibor wilayani Longido. Ambapo tukio hilo limetokea na kusababishwa na jamii ya wafugaji walio kuwa wakitorosha mifugo yao kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Aidha katika tukio hilo lililosababishwa na wafugaji hao wameweza kufanya uharibifu wa hali ya juu katika ofisi za serikali ya kijiji hicho pamoja na kupelekea kulazwa kwa afisa mmoja wa serikali baada ya kuumizwa na wafugaji hao.

Tukio hilo limetokea wakati wa uthaminishaji wa mifugo hiyo iliyo kamatwa hapo jana ikiwa katika hali ya kutoroshwa kupelekwa nchi jirani ya Kenya bila kulipiwa ushuru, jumla ya mifugo iliyo kamatwa ni ng’ombe 41 na mbuzi pamona na kondoo 521.

 Kwa upande wake mtedaji wa kijiji cha engarenaibor ndugu Tomath Ngobei ameeleza kuwa mifugo hiyo inakamatwa kwa sababu imekuwa ikipitishwa katika kijiji hicho kwenda nchi jirani ya kenya bila kulipiwa hivyo wamekuwa wakishirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi kuzuia utoroshwaji huo.

 Aidha Ngobei amesema uharibifu uliofanyika katika sehemu ya eneo la ghala la kuifadhia chakula ni kwa sababu eneo hilo ndilo walilo litumia kama chumba cha kumuhifadhi mmoja kati ya jamii hiyo ya wafugaji walio mkamata wakati wa ghasia hizo.

Utoroshwaji wa mifugo kupitia wilaya ya longido kupelekwa nchini Kenya umekuwa ukifanyika mara kwa mara na hivyo wizira ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na serikali ya kijiji, kata pamoja na tarafa wameungana kwa pamoja kuhakikisha swala hilo linafikia tamati.


from MPEKUZI

Comments