Upendo Peneza ataka REA iunde tume maalumu kusimamia miradi ya umeme

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), ameitaka Wizara ya Nishati kuunda kitengo maalumu cha kusimamia miradi ya umeme ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Mei 29 bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20 ambapo amesema kumekuwa na changamoto katika usimamizi wa miradi ya Rea. 

Aidha, mbunge huyo amehoji kuhusiana na mradi wa umeme wa Rufiji kwamba utatumia fedha nyingi wakati fedha hizo zingetumika kwenye miradi mingine kama ya jua.  

“Tumeambiwa itatumia miaka 10 ili lile bwawa liweze kujaa, Mheshimiwa Spika tunatumia hela nyingi kujenga mradi ambao utachukua muda mrefu na hautakuwa na faida.

“Maana yake tunataka kutengeneza historia kwani huo ni uharibifu wa fedha, tusipopata faida, tuna miradi ya jua na upepo, hizo trilioni 6.5 zilizotengwa, tungepeleka kwenye hiyo miradi mingine tungekuwa tuna umeme mwingi,” amesema


from MPEKUZI

Comments